DROO
ya michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 inayosimamiwa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF), inatarajiwa kufanyika Januari 15, jijini Nairobi,
Kenya.
Taarifa iliyotolewa na CAF Jumatatu, Januari 6, imeeleza kuwa
michuano hiyo itafanyika kuanzia Februari 1 hadi 28, 2025 nchini Tanzania,
Uganda na Kenya.
“Droo ya Mashindano ya Jumla ya (CHAN) 2024 itafanyika
katika Kituo cha Kimataifa cha Kenyatta jijini Nairobi, Kenya Jumatano, 15
Januari saa 20: 00 kwa saa za hapa nchini,”ilisema taarifa hiyo.
Mashindano hayo yanasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi
yametengwa kwa ajili ya wachezaji na ligi ya nchi husika kujitangaza kupitia
michuano hiyo.
Michuano ya CHAN itapambwa na mataifa kadhaa yenye nguvu katika
soka barani Afrika, wakiwemo mabingwa watetezi Senegal.