ZoyaPatel

Hatujasikia malalamiko yoyote ya ujazaji wa PEPMIS kwa Watumishi wa Afya – Deus Sangu

SohaniSharma

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (MB) Deus Sangu, amesema kuwa hakuna malalamiko yoyote ambayo wizara hiyo imepokea kuhusu ujazaji wa Majukumu yao ya kila siku katika mfumo wa PEPMIS na muingiliano wa majukumu yao ya kuhudumia wagonjwa.

Sangu ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma akijibu swali lililoulizwa na Mbunge, Sophia Mwakagenda, Mbunge wa viti maalumu aliyehoji Serikali ina mkakati upi wa kuwapunguzia majukumu ya ujazaji wa majukumu  watumishi wa sekta ya Afya kutokana na kuutumia muda mwingi kuhudumia wagonjwa, hivyo akaomba wajaze mara moja kwa mwezi badala ya wiki kama ilivyo sasa.

“Utaratibu wa upimaji watumishi kupitia PEPMIS tumeuweka kwa muda wa wiki kwa makusudi maalumu kwamba tuweze kulitambua tatizo ndani ya muda mfupi na kulitatua” amesema Naibu Waziri Sangu.

Hata hivyo ametilia mkazo kauli yake kuwa hakuna malalamiko yoyote yaliyojitokeza miongoni mwa watumishi wa Afya kuhusu uwepo wa changamoto katika ujazaji wa majukumu hayo kwa kile kinachoelezwa kuwa kikwazo cha wao kutotimiza wajibu wao wa kuhudumia wagonjwa.

 

 

 

Ahmedabad
Hyderabad
Previous Post Bangalore Next Post

نموذج الاتصال