Lagos, Nigeria | Juni 27, 2022, Mahakama Kuu ya Shirikisho ya jijini Lagos nchini Nigeria, ilikataa kusikiliza kesi zilizowasilishwa na Wakili wa Haki za Binadamu, Malcolm Omirhobo ambaye alifika mbele ya Mahakama hiyo akiwa amevalia mavazi yanayodaiwa kuwa na mfanano na yale ya Waganga wa jadi.
Wakili
Omirhobo, alitenda tukio wakati alipowasili katika Mahakama hiyo ya Juu, akiwa
na mchoro wa chaki nyeupe uliozunguka jicho lake moja huku akijifunga minyororo
kwenye miguu, kufunga kitambaa chekundu kiunoni mwake, kuvaa manyoya kichwani
na mkufu wenye kitu mfano wa hirizi.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama Kuu ya
Shirikisho, Tijani Ringim akiwa amevalia mavazi hayo Omirhobo alizua hisia
tofauti kutoka kwa baadhi ya mawakili waliodai kuwa hangeweza kusikiliza vyema
shauri lake, kitu ambacho kilizua mabishano kwa muda akidai alikuwa nadhifu.
Kesi ya kwanza ya
Omirhobo, ilikuwa ni ile dhidi ya Serikali ya Shirikisho ya Nigeria na nyinginezo
huku shitaka la pili likiwa dhidi ya Jeshi la Nigeria na watu wengine wawili,
ambapo iliitishwa na Jaji kisha kukataliwa kusikilizwa na kuahirishwa kitendo
alichokiita ni uvunjifu wa haki.
“Sheria
haziwezi kuchukua nafasi ya Katiba ya Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria, sioni
tatizo juu ya mavazi niliyovalia maana hayana uhusiano wowote na usikilizwaji
wa kesi hii, ukizingatia nipo nadhifu sasa kwanini kuna hisia tofauti,” alihoji
Omirhobo.