ZoyaPatel

Jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe

SohaniSharma

 


Vyakula vya kuku vinaweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa.

Chakula cha kuku ni lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile protini, wanga, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza kina mchanganyiko ufuatao:

 

·         Vyakula vya kujenga mwili kama vile jamii ya kunde, samaki, dagaa, mashudu ya ufuta, pamba na alizeti

·         Vyakula vya kulinda na kukinga mwili usipate maradhi kama vile mafuta ya samaki na majani mabichi kama kabichi, mchicha, majani ya mpapai na nyasi mbichi

·         Vyakula vinavyojenga mifupa kama vile aina ya madini, chokaa, mifupa iliyosagwa na chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama Kalishamu na Fosiforasi husababisha matege, kukunjamana kwa vidole, kufyatuka kwa misuli ya goti na kupofuka macho.

Maji ni muhimu sana kwani husaidia kulainisha na kurahisisha usagaji wa chakula, na kupunguza joto. Wakati wa joto kali kuku wapewe maji mengi.

Kabla ya kutengeneza chakula lazima mtengenezaji ajue haya:

·         Jinsi ya kupata vyakula vya aina mbali mbali

·         Kiasi cha viinilishe vinavyohitajika kwa kuzingatia umri na aina tofauti ya kuku; kwa mfano vifaranga wanahitaji protini asilimia 18 hadi 22, kuku wanaokua asilimia 17 hadi 19 na kuku wa mayai asimilia 15 hadi 17. Vile vile madini aina ya Kalishamu kiasi cha asilimia tatu hadi nne kinahitajika kwa kuku wa mayai na asilimia moja kwa kuku wa nyama na vifaranga.

·         Viwango vya uchanganyaji wa aina za vyakula mbali mbali. Ili mtengenezaji aweze kutengeneza chakula bora ni muhimu afuate kiwango cha uchanganyaji

Kilichopendekezwa. Kiasi cha aina moja ya chakula kinapozidi kinaweza kuleta madhara.

Jedwali lifuatalo linaonesha kiwango kinachotakiwa kwa baadhi ya vyakula.

1.        Vyakula na viwango vinavyohitajika kwa asilimia 100

Aina ya Chakula

Kiwango cha uchanganyaji (%)

Vyakula

Vifaranga

Kuku wa nyama

Kuku wa mayai

Mahindi

70

70

70

Ulezi

20

40

40

Mtama

20

30

30

Mpunga

40

70

70

Ngano

5

40

40

Pumba za mahindi

10

20

20

Pumba za mpunga

10

20

20

Pumba za mtama

10

20

20

Pumba za ngano

5

15

15

Mashudu ya nazi

10

30

40

Mashudu ya pamba

5

10

5

Mashudu ya alizeti

10

20

20

Mashudu ya ufuta

10

10

5

Damu iliyokaushwa

5

5

5

Mifupa iliyosagwa

5

5

7.5

Dagaa

10

5

5

Lusina iliyosagwa

(Lucerne meal) Lukina

5

5

5

Lcuecana meal

2.5

5

5

Chokaa

5

5

5

Chumvi

0.5

0.5

0.5

Soya

10

20

20

 

·         Kuhusu kiasi cha viinilishe kama protini, wanga, madini na vitamini vilivyomo kwenye aina za vyakula vitakavyochanganywa, Mfugaji anashauriwa amuone mtaalamu wa mifugo aliyekaribu naye aweze kumpa ushauri zaidi.

·         Mchanganyiko uwe na zaidi ya aina moja ya vyakula kwa mfano vyakula vya kujenga mwili vitokanavyo na wanyama na mimea.

 

1.        Mfano wa kutengeneza kilo 100 za chakula cha kuku;

Vyakula

Kiasi (Kg)

Mahindi

30.00

Pumba za mahindi

20.00

Soya

18.00

Mashudu ya alizeti

20.50

Dagaa

5.00

Mifupa iliyosagwa

4.00

Chumvi

0.50

Vitamini

2.00

Jumla

100.00


1.        Mfano wa chakula cha kukuzia kuanzia juma la nne hadi la nane

Vyakula

Kiasi (Kg)

Mahindi

45.00

Pumba za mahindi

20.00

Mashudu ya pamba

5.00

Soya

20.00

Dagaa

2.50

Mifupa iliyosagwa

5.00

Chumvi

0.50

Vitamini

2.00

Jumla

100.00

 

1.        Mfano wa chakula cha kuku wa mayai kuanzia juma la nane hadi la ishirini

A

B

Vyakula

Kiasi (Kg)

Vyakula

Kiasi (Kg)

Mahindi

45.00

Mahindi

45.00

Pumba za mahindi

25.00

Pumba za mahindi

30.00

Soya

5.00

Soya

5.00

Mashudu ya alizeti

10.00

Mashudu ya pamba

5.00

Dagaa

4.00

Dagaa iliyokaushwa

4.00

Damu

3.00

Mifupa iliyosagwa

2.50

Chokaa

3.00

Chokaa

3.00

Chumvi

0.50

Chumvi

0.50

Vitamini

2.00

Vitamini

2.00

Jumla

100.00

Jumla

100.00

 

1.        Mfano wa chakula cha kuku wa mayai kuanzia wiki ya ishirini na kuendelea

A

B

Vyakula

Kiasi (Kg)

Vyakula

Kiasi (Kg)

Mahindi

50.00

Mahindi

40.00

Pumba za mahindi

15.00

Pumba za mahindi

25.00

Mashudu ya pamba

5.00

Mtama

5.00

Soya

18.00

Mashudu ya alizeti

10.00

Dagaa

4.50

Dagaa

4.00

Mifupa iliyosagwa

3.00

Damu iliyosagwa

5.00

Chokaa

2.00

Mifupa iliyosagwa

4.50

Chumvi

0.50

Chokaa

4.00

Vitamini

2.00

Chumvi

0.50

Jumla

100.00

Vitamini

2.00

 

 

Jumla

100.00

 

Ahmedabad
Hyderabad
Previous Post Bangalore Next Post

نموذج الاتصال