Serikali imeahidi kutekeleza kanuni ya kupitisha uvuvi wa samaki aina ya Mgebuka kwa kutumia wavu aina ya makila.
Majibu hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Mizengo Pinda, kwa niaba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa swali lililoulizwa na Mbunge wa Kigoma mjini Kilumbe Shaban Ng’enda, akitaka kujua upi mwelekeo wa serikali katika kuboresha kanuni ya uvuvi ili kupata ufumbuzi wa aina ya wavu wa kuvulia samaki aina ya Migebuka.
Akijibu swali lililoulizwa leo Januari 28 Bungeni Dodoma Naibu Waziri Pinda amesema kuwa maboresho ambayo yamekuwa yakifanyika kwa kanuni ya uvuvi ya mwaka 2009, ambapo 2019 na 2020 yalifanyika maboresho ya kanuni hiyo ili kukidhi mahitaji ya shughuli za uvuvi nchini,
Amesema kuwa serikali ipo mbioni kutoa waraka wa matumizi ya
wavu wa makila kwa uvuvi wa samaki aina ya mgebuka katika ziwa Tanganyika ili
kuondoa adha na changamoto wanayoipata wavuvi wa ziwa Tanganyika.