Magoli yake mawili dhidi ya Tp Mazembe yamefanya idadi ya mabao yake katika Ligi ya Mabingwa msimu huu kufikia matatu katika mechi tatu alizocheza (huku mechi mbili akianza), na yameweka hai matumaini ya Yanga kufuzu hatua ya robo fainali.
Goli lake la kwanza lilikuwa shuti la mbali la kuvutia kutoka mita 30, lililoelekea moja kwa moja kwenye kona ya juu ya wavu ambalo lilisawazishia Yanga kabla ya kufunga goli la pili na kutoa pasi ya mwisho iliyozaa goli moja huku Aziz Ki akiifungia Yanga goli moja na kuweka idadi ya goli 3 – 1 katika mechi ya nne ya hatua ya makundi iliyopigwa wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.
Ahmedabad
Tags
Michezo Kitaifa