Fort Lauderdale, Florida:
Miili ya watu wawili imegunduliwa
katika sehemu ya magurudumu ya ndege ya shirika la JetBlue iliyotua katika
Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale-Hollywood, Florida, ikitokea Uwanja wa Ndege
wa JFK, New York.
Kwa mujibu wa taarifa za shirika hilo, miili hiyo iligunduliwa Jumatatu
jioni, Januari 6, wakati wa ukaguzi wa kawaida wa matengenezo baada ya safari
ya ndege.
JetBlue ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema:
"Jumatatu jioni, Januari 6, katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale-Hollywood,
watu wawili waligunduliwa katika sehemu ya magurudumu ya moja ya ndege zetu
wakati wa ukaguzi wa kawaida baada ya safari. Kwa masikitiko makubwa, wote
walikuwa wamefariki."
Hadi sasa, haijajulikana kwa namna gani wa watu hao waliweza kuyafikia
magurudumu ya ndege hiyo.
JetBlue imesema inashirikiana kwa karibu na mamlaka husika kusaidia katika
uchunguzi wa tukio hili.
"Tukio hili ni la kusikitisha sana, na tumejitolea kushirikiana kwa ukamilifu na mamlaka ili kuelewa kilichotokea," JetBlue iliongeza
Mamlaka za usalama wa anga zinaendelea kuchunguza tukio hili ambalo limezua
maswali kuhusu usalama wa ndege na jinsi watu walivyoweza kuingia katika sehemu
ya magurudumu bila kugunduliwa.