Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga leo Februari 10, Bungeni
jijini Dodoma ameitaka serikali kutenga bajeti ya kutosha ili kuhakikisha maeneo
yenye uzalishaji katika Wilaya ya Ludewa yanapata umeme wa kutosha ili
kuondokana na adha ya kukatika kwa umeme na hivyo kuathiri shughuli za
uzalishaji.
Kamonga ameelekeza swali kwa Naibu Waziri wa Nishati, Judith
Kapinga ambaye amekiri uwepo wa tatizo hilo huku akiweka bayana kuwa serikali
mwanzoni ilifanikiwa kutuma wataalamu kwa ajili ya kufanya uhakiki pamoja na
gharama itakayotumika kwa ajili ya kubadilisha miundombinu.
Naibu Waziri amemhakikishia Mbunge Kamonga kuwa serikali
itaendelea kutafuta fedha kwaajili ya kufanya marekebisho katika maeneo ya uzalishaji
ili wananchi wa Ludewa waendelee kuwa sehemu ya wanaufaika wa umeme kupitia
uzalishaji wao.