ZoyaPatel

Rais Samia ataka usawa katika utoaji haki

SohaniSharma



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Mahakama inapaswa kuwa chombo cha kuhamasisha shughuli za kiuchumi kwa kuhakikisha inatenda haki kwa usawa na kwa wakati.

Dkt. Samia ameyasema hayo leo, Februari 3, 2025, alipozungumza na Majaji, wageni waalikwa, na wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Amesema, “Mahakama inatakiwa kuwa chombo cha kuhamasisha shughuli za kiuchumi kwa kutenda haki kwa usawa na kwa wakati. Kauli mbiu hii, 'Tanzania ya 2050, nafasi za taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya maendeleo,' inanipa faraja kwamba agizo langu nililolitoa wakati nilipopokea taarifa ya kamati ya kuangalia taasisi ya haki jinai sasa linakwenda kufanyiwa kazi.”

Awali, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, alisisitiza umuhimu wa kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya Mawakili na Mahakimu, akieleza kuwa hili litasaidia kuboresha huduma kwa wananchi.

“Kweli, majengo ni ya kuvutia na teknolojia ni nzuri, lakini ni muhimu pia kuhakikisha tunaboresha maslahi na mazingira yao, kwa sababu ni hatari kwa mwananchi mwenye shida kukutana na wakili mwenye changamoto za kipato na hakimu mwenye hali ya kifedha isiyokuwa nzuri. Hapa anayeshughulikiwa ni mwananchi, hivyo kuboresha hali zao kutakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi,” alisema Wakili Mwabukusi.

Ahmedabad
Hyderabad
Previous Post Bangalore Next Post

نموذج الاتصال