ZoyaPatel

SIMULIZI: Chozi la Mwanaume | Sehemu ya Kwanza (1)

SohaniSharma

 


Ni simulizi  inayohusu binti na kijana mmoja waliokuwa wakiishi huko Shinyanga miaka ya Nyuma.

Kijana alikuwa tu mkulima na binti alikuwa Muuguzi.

Siku moja wakiwa katika Daladala kila mmoja akitoka kwenye mizunguko yake, ndipo kijana akamwona yule binti ambaye alikuwa akitoka Zahanati na kurejea nyumbani baada ya msongo wa mawazo mwingi uliotokana na kazi nyingi ile siku.

Kijana akamsalimia Nesi habari yako; hakumjibu badala yake alimuangalia kuanzia juu hadi chini kwa ishara ya kuonesha yule kijana hakuwa na sifa ya kumsemesha yule binti.

"Ninakusalimia Dada, salamu ni jadi yetu" aliongea yule kijana akionesha hakufurahishwa na kile kitendo cha yule binti.

Ulifika muda wa yule binti kushuka kituo cha daladala na alipojisachi kwenye pochi yake kumbe alisahau nauli yake alimwazima rafiki yake, kwa makubaliano ya kumrudishia wakati wa kurudi kutoka kazini.

Yule kijana aliyekuwa ametoka shambani akajibu kwa ustaarabu tu, "Konda endelea na safari nauli nitalipa mimi"

Yule Dada hakujibu chochote aliondoka na yule kijana akaendelea na safari yake.

Zilipita kama siku tatu yule kijana alijisikia kuumwa, na ilikuwa dalili ya Homa, hivyo akaamua kwenda Zahanati ya Shauri Moyo, ambayo ilikuwa umbali mdogo kutoka nyumbani kwao, lakini aliamua kwenda hapo kutokana na sifa nzuri ambayo Zahanati hiyo ilikuwa imejijengea.

Alifika Zahanati ya Shauri Moyo, Manispaa ya Shinyanga na alipotia mguu wake mlangoni, ghafla alimwona yule binti aliyegoma kuitikia salamu ya yule Kijana, akaamua tena kumsalimia; 

John: Dada habari

Esther: Poa,

John: Naitwa John, tulikutana kwenye daladala kama siku tatu zimepita, unanikumbuka?

Esther: Kwahiyo jukumu langu ni kumkariri kila anayepanda Daladala?

John: Sijamaanisha hivyo Dada, samahani kama nimekukwaza

Esther: Unaonekana una malaria wewe sio bure, maana huwezi ukaja sehemu kama hii unaulizia habari ya kukutana kwenye daladala

John: Ni kweli naumwa, japo sijui kama ni malaria au shida gani, lakini sio sababu ya mimi kukuuliza hivyo, ndio maana nimeomba samahani.

Esther: Ugua pole; 

Esther akaondoka huku akibinua midomo yake kama ishara ya kuonesha hakufurahishwa na maswali ya John

John alitibiwa na kuondoka katika ile zahanati lakini alishuhudiwa moyoni kuwa alikuwa ndege aliyenasa kwenye ulimbo na hakujua anajinasua vipi.

Huku Esther naye, baada ya pilipilika aliamua kukaa katika moja ya mabenchi ya zahanati aweze kupumzika, ndipo alimfuata Muuguzi mwenzake, Mama wa Makamo aliyeheshimika sana katika ile zahanati maarufu kwa jina la Mama Ushauri, walianza mazungumzo.

Mama Ushauri; Mwanangu unaonekana hauko sawa, tangu asubuhi sikuoni kama nilivyozoea kukuona siku zote shida nini?

Esther: Mama Ushauri kuna kijana amekuja leo, yule kijana toka nimemuona siku ya kwanza kwenye Daladala sikumpenda lakini anaonekana king'ang'anizi sana kwangu.

Kwanza mchafu, anaonekana haogi na nguo hafui pia, kama ulivyomwona ndefu kama steel wire, sitaki kumwona ananichefua.

Mama Ushauri: (Akicheka) unajua moyo wako ndio unaoongea vile unavyomchukulia, lakini yeye kwake hakutafsiri hivyo! kwani amekutongoza hadi useme hivyo?

Esther; Hapana, lakini vimaswali maswali vyake sivipendi, vinaniboa sana

Mama Ushauri; Sikiliza mwanangu. Utu wa nje hautoshi kueleza usafi wa mtu.

Kuna watu ni wasafi nje, wananukia marashi lakini roho zao ni majitaka yasiyofaa hata kupita mtaroni, na kuna watu ni wachafu kwa nje lakini ndani yao, mioyo yao imepambwa na dhahabu ya utu na heshima.

Naomba nikuulize mwanangu, kipi unahisi kinakukwaza zaidi kuhusu yeye?

Esther: Ni mchafu mchafu muda wote, sipendi, na sitaki anizoee pia.

Mama ushauri; akija mwambie kuwa haufurahishwi na anavyovaa, uchafu wake na haupendi aendelee kukutana na wewe.

Esther: Sawa Mama, alijibu na kubeba mkoba wake kisha kuelekea kituo cha Daladala

Akiwa anaelekea kupanda Daladala aliambatana na Rafiki yake aliyejulikana kaa jina la Loswita, wakaendelea kupiga stori za hapa na pale.

Esther; Loswita hivi unajua mkiwa chumba cha Labour kuna Mkaka alikuja hapa mchafu mchafu, akaanza kuniuliza maswali, basi yule kama nakuambia nimemkomesha na vimaswali vyake!

Loswita: Mwenzangu nimekuona wakati naenda kuchukua bandeji nikajiuliza mwenzetu kamtoa wapi muokota makopo kutuletea hapa Zahanati?

Hahaha! wakacheka, kisha wakapanda daladala, wakiwa kwenye Daladala

Loswita: Enhee mwenzangu, kwahiyo kasemaje, Anakupenda?

Esther; Si bora angeniambia hivyo ningejua ana utimamu, kaanza kuniuliza ooh, sijui tulikutana kwenye daladala sijui hivi mara vile, nikamwambia wewe una malaria, na kweli kapimwa kakutwa ana malaria. 

hehehe! wakacheka wakagonga mikono huku kila mmoja mkono mmoja umeshikilia chuma kwenye Daladala.

Siku iliisha na ikafuatia siku nyingine ya kuwajibika kazini.

Zilipita siku tano John alirudi Zahanati kwa ajili ya kujua hali ya maendeleo yake, ghafla Esther, alipomwona akafichama ili John asimwone.

Alifika hadi eneo la mapokezi akaulizia samahani kuna binti yuko hivi na hivi, wakatambua alikuwa Esther akatafutwa asionekane 

ITAENDELEA........

Ahmedabad
Hyderabad
Previous Post Bangalore Next Post

نموذج الاتصال