ZoyaPatel

SIMULIZI: Chozi la Mwanaume | Sehemu ya Pili (2)

SohaniSharma

Alikuwa kajificha nyuma ya mlango wa choo cha watumishi wa zahanati.
Alikaa kama Dakika 25 John akawa ameondoka lile eneo.

Siku iliyofuata John aliamua kwenda katika ile Zahanati, mahususi kwa ajili ya kutaka kumwona Esther na kuzungumza naye, hasa kwa kuweka hisia zake wazi kuwa alikuwa ameshampenda na alitamani wawe na mipango ya pamoja na ikiwezekana wafunge ndoa.

Alifika John na kukutana na Mama Ushauri, alisalimia kwa adabu na unyenyekevu

John: Mama shikamoo
Mama Ushauri: Marahaba mwanangu, karibu nikusaidie jambo gani?

John: Mama nimekuja nina shida binafsi na mhudumu wa Afya, kuna ujumbe wake nimemletea

Mama Ushauri; anaitwa nani?

John: Ni... ni... 

Mama Ushauri: Alicheka kwa kigugumizi cha John, kisha akauliza, hata jina haumfahamu?
John: Ndio mama ni mweupe, hajasuka, ni mnene wa wastani, ana macho ya kizungu

Mama Ushauri: Esther! Esther, aliita mara mbili Mama ushauri na Esther akatokea mbele ya John, ni Mgeni wako anasema ana ujumbe wako, kazungumze naye aliongea mama ushauri akiwa ameinamia karatasi ya Mgonjwa aliyekuwa akimjazia fomu ya matibabu.

Esther alitoka na kwenda kusimama pembezoni mwa moja ya miti iliyokuwepo katika zahanati hiyo huku John akimfuata kwa nyuma:

Enhee! nakusikiliza aliongea Esther akiwa mwenye jazba kali
... kwanza samahani Dada nimekuja muda ambao upo kazini;
...... ishia hapo hapo, alijibu Esther, kama ujumbe wako hauhusiani na kazi pita hivii

Hapana naomba nisikilize Esther, aliongea John kwa hisia, akitaka kupiga magoti

..... weee weee weee! umesahau hapa ni Zahanati, umesahau mimi mtumishi wa Umma unataka nifukuzwe kazi, ishia hapo hapo
...... lakini Esther, aliongea John akionesha sura huzuni, haya sema alimkatisha Esther.
ITAENDELEA......
Ahmedabad
Hyderabad
Previous Post Bangalore Next Post

نموذج الاتصال