ZoyaPatel

Wastaafu walioathiriwa na Kikokotoo wanayo nafasi ya kulipwa fidia zao

SohaniSharma

 


Wastaafu walioathirika na mchakato wa mabadiliko ya kikokotoo cha pensheni, wametakiwa kuwasilisha taarifa zao kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ili malalamiko yao yaweze kufanyiwa kazi.

Akizungumza leo Februari 10 Bungeni jijini Dodoma katika Mkutano wa 18 na kikao cha 10, Waziri mwenye dhamana Ridhiwani Kikwete amelieleza Bunge kuwa serikali imeshajipanga na ipo tayari kuwasilikiliza wastaafu hao pamoja na kurekebisha taarifa zao kwa wale ambao hawajarekebisha ili waendelee kupata stahiki zao kama ilivyo kwa wengine.

Wito huo umekuja baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Christina Mnzava kuitaka serikali kutoa tamko juu ya wastaafu walioathirika na kikokotoo na hivyo kutolipwa fidia kwa athari ya mabadiliko yaliyokuwepo huko nyuma.

Waziri Ridhiwani Kikwete amesema “Wale watu wote ambao wana madai yoyote, yanayoendana na madai ya kikokotoo, kutokana na sintofahamu aliyoizungumza Mbunge; lakini pia wale ambao taarifa zao hazijakaa vizuri; ningeomba ziwasilishwe katika ofisi yetu ili tuweze kuzifanyia kazi.

Pia akaongeza kwa kusema kuwa “ Serikali ya awamu ya sita kama awali nilivyoeleza; kitendo cha kuongeza kutoka laki 1 hadi laki 1 na nusu ni wazi na inaonesha kuwa mambo yetu ya kiuchumi yamekaa vizuri na Mhe. Rais yupo tayari kusaidia wale wote wenye mahitaji na matatizo katika maeneo hayo.

Awali akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Rashid Shangazi, Mbunge wa Mlalo kuhusu usumbufu wanaoupata wastaafu wengi kufuatilia madai yao katika Ofisi za Wilaya na Mkoa na ufanyaji tathmini wa pensheni zao, kwa kile alichoeleza wastaafu wengi kutokuwa vizuri kiafya na kuishi pembezoni.

Waziri Kikwete amesema Serikali Kuu kwa kushirikiana na Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Mkoa, wanaandaa utaratibu maalumu utakaowezesha wastaafu kufikiwa moja kwa moja katika maeneo yao badala ya kusafiri ili kuwaondolea usumbufu.

Ahmedabad
Hyderabad
Previous Post Bangalore Next Post

نموذج الاتصال