ZoyaPatel

Watu zaidi ya 300 wanatibiwa na Kitengo cha Fiziotherapia, Njombe RRH kwa mwezi

SohaniSharma



Watu wapatao mia nne wamekuwa wakipatiwa huduma katika Kitengo cha Fiziotherapia chini ya Idara ya Utengamao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Idara ya Utengamao, Rasuli Chihako, ambaye amesema uwepo wa vifaa vya kisasa umechangia kwa kiasi kikubwa kuwanufaisha wananchi wa mkoa wa Njombe kupata huduma bora katika kitengo hicho.

Miongoni mwa changamoto zilizotajwa kuwa kubwa kwa wananchi waliofika kupata eneo hilo ni pamoja na Maumivu ya Mgongo na Mguu Kifundo (nyayo zilizopinda) kwa watoto.

Mathalani; ubebaji wa mizigo na utuaji usiofaa, ukaaji usio sahihi mahali pa kazi na majumbani,kufua na kudeki ukiwa umeinama vimetajwa kuwa kichocheo cha watu wengi kupata shida ya migongo kuuma, maumivu kwenye maungio na misuli.

Rasuli, ameshauri jamii kuepukana na kubeba vitu vyenye uzito wa kupitiliza, kufuata njia bora za unyanyuaji na utuishaji wa mizigo, kuzingatia ukaaji mzuri hasa mahali pa kazi na kufika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ili kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu mtindo wa maisha. 


🫱BONYEZA HAPA KUTAZAMA ZAIDI

Ahmedabad
Hyderabad
Previous Post Bangalore Next Post

نموذج الاتصال