Mwanasiasa na Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo
Zitto Kabwe amesema uamuzi wa Trump kusitisha misaada dhidi ya nchi za Afrika
una uhusiano wa moja kwa moja na kuokoa uchumi wa Taifa lake na kurejesha nguvu,
kwa kile alichoeleza tishio la ukuaji kwa kasi wa uchumi wa China.
Zitto Kabwe akipiga stori na Power Breakfast ya Clouds FM
leo Februari 12, amesema kuwa hakuna shaka kuwa kwa sasa China ni Taifa lenye
nguvu kubwa duniani ila kinachoitofautisha na mataifa ya Magharibi kama
Marekani ni kuwa China haipendi kuingilia mataifa mengine.
Ametumia ishara mbalimbali ikiwemo kukua na kujitosheleza kwa uchumi wa Taifa la China, nguvu ya kijeshi na Diplomasia iliyopanuka kuwa sababu za kuifikiria kwa ukubwa huo.
China limekuwa ni Taifa ambalo lipo kwenye fikra za wanasiasa wengi wa Marekani kwa sababu ya kasi yao ya ukuaji wa uchumi, namna wanavyoshikLria mnyororo wao wa ugavi, na sasa tunazungumzia ukuaji wa teknolojia ambayo imewekezwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa madini mkakati, na hivyo kuwa na bidhaa kama magari ya umeme, na malighafi mbalimbali, hiyo ndio sababu Marekeni na mataifa ya Ulaya yanafanya kila njia kuanzisha sera za uwekezaji ambazo zinambana China. Amenukuliwa Zitto Kabwe
Ameongeza kuwa usitishaji wa misaada Barani Afrika na kwingineko
duniani utakuwa na athari ya moja kwa moja kwa Marekani kupoteza ushawishi.
Leo hii Marekani akija Tanzania na ana jambo lake ana kipi cha kushawishi ikiwa hatoi msaada wowote ..Marekani ameacha mlango wazi hivyo China ataingia na kuleta hata modeli yake ya Demokrasia kwa sababu atakuwa na hiyo nguvu ambayo Marekani aameipoteza. Amesema KabweAhmedabad
Tags
Duru za Kimataifa