Wizara ya Maliasili na
Utalii imetunga Kanuni za Usimamizi wa Shughuli za Uvuvi katika maeneo ya
Hifadhi za wanyamapori (Mapori ya Akiba na Tengefu).
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati akiwasilisha
hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026
ambapo amesema tangazo hilo zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Namba. 781
la mwaka 2024.
Amesema,
“Kanuni za Biashara za Nyara zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na. 884 la
mwaka 2024, na Kanuni za Utalii wa Picha zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali
Na. 875 la mwaka 2024. Vilevile, Wizara imefanya mapitio ya Kanuni za Uwindaji
wa Kitalii zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na. 780 la mwaka 2024 na
Kanuni za Usimamizi wa Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) za
mwaka 2018.
“Sambamba na hilo,
Wizara imeandaa Mipango ya Jumla ya Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori
(General Management Plan) ya Jumuiya za ISAWIMA (Kaliua), Ifinga (Madaba),
Uyumbu (Urambo), na UKUTU (Morogoro). Katika hatua nyingine, Wizara imeandaa
Mwongozo wa upatikanaji wa mazao ya wanyamapori na mimea inayosimamiwa na
Mkataba wa CITES ili kuimarisha utekelezaji wa mkataba huo”. Amesema Dkt. Chana
Amesema Kanuni hizi
zinalenga kuimarisha uhifadhi shirikishi na matumizi endelevu ya rasilimali za
wanyamapori.
“katika kukabiliana
na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu, Wizara imeendelea kutekeleza
Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa Utatuzi wa Migongano kati ya Binadamu na
Wanyamapori”, amesema
“Katika
kutekeleza Mkakati huo, Wizara kupitia TAWA, TANAPA na TAWIRI imekamilisha
ujenzi wa vizimba 12 vya kudhibiti mamba na viboko katika Halmashauri za Wilaya
za Bunda (3),Korogwe (1), Ludewa (2), Uvinza (2), Tandahimba (2), Nanyumbu (1)
na Mkinga (1)”. Amesema Dkt. Chana
Hata hivyo
amesema, ujenzi wa vizimba sita (6) unaendelea katika Wilaya za Buchosa (2),
Sengerema (1), Bunda (1), Newala (1) na Kibiti (1). Vizimba hivyo vitasaidia
kuimarisha usalama wa wananchi wanaotumia maji ya mito na maziwa katika maeneo
hayo.